KOCHA wa Tanzania Prisons, Mohammed ‘Adolf’ Rishard, amesema hawatakubali rekodi yao ya kutokufungwa kwenye Ligi Kuu ivunjwe na Yanga kwenye mchezo utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Tanzania Prisons ambayo imecheza michezo 13 na kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 na ikiwa imeshinda mechi tano, sare michezo nane, inakutana na Yanga inayoshika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 18.

Adolf Richard ametoa tahadhari hiyo kwa Yanga ikiwa ni siku moja baada ya kupunguzwa kasi kwa kugawana pointi na Mbeya City kwenye mchezo wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja Sokoine ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa kesho.

“Tumejijengea falsafa moja ya kuwaheshimu wapinzani na tutaindeleza kwa Yanga ila wasije wakatarajia watakuja kupata matokeo kirahisi.

"Baada ya kutoka sare mechi iliyopita hatuwezi kukubali rekodi ya kutokufungwa ivunjwe na Yanga tena katika uwanja wetu wa nyumbani,” alisema.

Alisema wanaiheshimu Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wazoefu na wenye uwezo wa kubadilisha matokeo wakati wowote, lakini kupitia mechi iliyopita wameona udhaifu wao mwingi, hivyo wamejipanga kuhakikisha dakika 90 zitaamua mshindi kuwa wao.

“Wachezaji wote wako fiti kwa mchezo, kikubwa tubaomba mashabiki wa Mbeya na sehemu za jirani kujitokeza kwa wingi kutushangilia kwani ushindi wetu ni sifa ya mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini,” alisema Adolf Richard.

Alipotafutwa kocha wa Yanga, Charles Mkwasa, kuzungumzia maandalizi ya mchezo dhidi yaTanzania Prisons, aligoma kuzungumza kwa madai yupo kwenye mapumziko ya sikukuu ya Krismasi.

“Kama unataka taarifa kuhusu maandalizi ya timu kujipanga na mchezo ujao mtafute Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, atakuambia lakini kwa sasa nimechoka na sitaki kuongelea maana nipo mapumziko nasheherekea sikukuu ya Krismasi hapa Mbeya,” alisema Mkwasa

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.