Inaelezwa kuwa uongozi wa Yanga uko kwenye harakati za kumalizana na straika Tariq Seif kutoka Dekernes FC ya Misri.
Mabosi wa mabingwa hao wa kihistoria kunako Ligi Kuu Bara wameanza mchakato wa kupata saini yake ikiwa zimesalia siku chache kuelekea dirisha dogo.
Kuna uwezekano Seif akamalizana na Yanga kesho kwa kutambulishwa rasmi na wakati akimalizana na wakongwe hao, Seif amefanikiwa kuingia kambani mara tano tangu asajiliwe na waarabu hao.
Mbali na kufunga mabao matano, Seif amefanikiwa kutengeneza nafasi tatu za kufunga.
Post a Comment