Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji ‘MO’,  amewaahidi wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kitita cha Sh. milioni 100 na bodaboda ikiwa watatwaa ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoendelea nchini Uganda.

Dewji ametoa ahadi hiyo katika kambi ya Kilimanjaro Stars aliyoitembelea usiku wa juzi kwa ajili ya kuwapa hamasa akiwa nchini Uganda.

“Naamini mtafanya vizuri katika michezo yenu iliyobakia na mimi nawaahidi kuwapa zawadi ya Shilingi 100 milioni na pikipiki kwa kila mchezaji,” alisema Dewji.

Stars ilishuka dimbani jana dhidi ya Zanzibar Heroes ambapo iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 likiwekwa kimiani na Ditram Nchimbi.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.