Wakati tambo za watani wa jadi zikiwa zimeanza kushika kasi, Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda, amewatahadharisha Yanga kujipanga kuelekea mechi hiyo.

Simba itakutana na Yanga mwakani Januari 4 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mechi ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake.

Kaduguda amewapa tahadhari Yanga kwa kuwaambia wamalize migogoro yao mapema ili waepuke kukutana na kichapo cha maana.

Amewaomba wawe na tahadhari kwani wao wanazidi kujipanga na akiwaomba endapo wakifungwa wasije kusema sababu tulikuwa na migogoro.

"Tunawaomba wenzetu wajiandae vizuri kwani sisi tuko katika maandalizi.

"Vema wakamaliza migogoro yao haraka ili baadaye wasije leta visingizio kuwa wamepoteza kwa kuwa hawako vizuri."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.