Imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtaka beki wa Yanga, Andrew Vincent 'Dante' kurejea mara moja kazini kwa mwajiri wake.
Taarifa zinasema kuwa mabosi wa Yanga waliamua kukata rufaa dhidi ya mchezaji huyo ambaye aliamua kugoma kutokana na kudai stahiki zake.
Dante ambaye aligoma naye alifungua kesi TFF akiomba alipwe fedha zake ambazo ni zaidi ya milioni 45.
Licha ya kushitaki, Yanga nao walikata rufaa ya kutaka wamalizane wao kwa wao na inaelezwa TFF wameamua arejee kazini ili wakamalizane wenyewe.
Tangu msimu huu uanze, Dante ameshindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa takribani robo tatu ya mechi ambazo imecheza msimu huu.
Post a Comment