Mchezaji wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza EPL, Neil Shipperley (45) amehukumiwa kifungo cha nje kwa miezi 12 kwa kosa la kujichua (Masturbation) mbele ya mkewe na mtoto wake.
Shipperley ambaye aliwahi kucheza katika klabu za Southampton, Crystal Palace, Chelsea na Wimbledon alifanya tukio hilo Septemba 17, 2019 alipokuwa kwenye gari pamoja na mkewe na mtoto wake mwenye umri wa miaka 16.
Aliwavusha wawili hao kukatiza barabara lakini ghafla naye alishuka kutoka kwenye gari huku akiwa ameshika tupu yake akielekeza kwao.
Amepewa hukumu ya miezi 12 ya nje kufanya shughuli za kijamii (community orders) ambapo siku 20 atazitumia kwa matibabu ya kisaikolojia, ikiwa ni maagizo ya mahakama.
Pia anatakiwa kufanya kazi kwa muda wa saa 120 bila malipo pamoja na kulipa faini ya pauni 200 ambayo ni sawa na sh. 603,400 kwa waathirika wa tukio hilo kama fidia.
Post a Comment