Tunaweza kusema mabingwa wa kihistoria katika soka la Tanzania kwa upande wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wanapitia wakati mgumu kutokana na madeni wanayodaiwa na wachezaji wao.

Achana na Lamine Moro, David Molinga, Juma Balinya na Sadney Urikhob ambao wanatajwa kuondoka kutokana na kutolipwa stahiki zao, Yanga bado ina mtihani wa Anderw Vicent 'Dante'.

Mtihani unatokana na deni lake la shilingi za Kitanzania, milioni 45 ambazo bado anadai mpaka sasa.

Dante anadai fedha hizo zikiwa zimeunganika zile za mshahara na usajili, mchezaji huyo anaidai Yanga na miezi kadhaa sasa hajafanya kazi ya kuichezea timu yake mpaka alipwe.

Uzito wa madeni ambayo kiuhalisia Yanga imeyumba kiuchumi hivi sasa unaipa wakati mgumu klabu hiyo ambayo ukiachana na Simba, ni kongwe katika soka la Tanzania.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.