Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utalitolea ufafanuzi wa kina suala la wachezaji wake wa kigeni kuondoka klabuni hapo.
Juzi zilienea taarifa za wachezaji Lamine Moro, David Molinga, Juma Balinya na Sadney Urikhob kutangaza kuachana na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga, Kariakoo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Hassan Bumbuli, amesema watalitolea ufafanuzi wa kina leo na akiwataka wanayanga kutulia akisema kila kitu kitakuwa sawa.
Bumbuli ameeleza wataeleza kila kitu na mustakbali mzima wa wachezaji hao ambao wametekea vyombo vya habari katika medani za soka hivi sasa.
Post a Comment