Kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm amethibitisha kutuma barua ya kuomba kazi ndani ya timu hiyo wiki mbili zilizopita kurithi mikoba ya Mwinyi Zahera aliyetimuliwa mwezi uliopita. Imeelezwa.

Zahera ambaye kwa sasa yupo hapa nchini kudai stahiki zake alifungashiwa virago baada ya timu hiyo kuboronga kwenye mechi za kimataifa na zile za Ligi Kuu Tanzania Bara na kikosi hicho kukabidhiwa kocha wa muda Charles Mkwasa.

Pluijm aliyekinoa kikosi hicho kwa mafanikio makubwa kwa misimu ya nyuma na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara alisema licha ya mambo yanayoendelea kwenye timu hiyo ikiwemo baadhi ya wachezaji kuhusishwa kuondoka kutokana na matatizo ya stahiki zao haimkatishi tamaa.

Taarifa imesema kuwa, Hans amethibitisha hilo na kudai hadi sasa mipango ya mawasiliano na uongozi wa timu hiyo inaenda vyema .

Imeenda mbali kwa kueleza wakati anakinoa kikosi hicho alikuwa anafanya kazi kwa uhuru mkubwa ikiwemo kupata ukarimu kutoka kwa mashabiki na ushirikiano kutoka kwa viongozi sambamba na wachezaji hadi kupata mafanikio na hicho ndicho kinachozidi kumpa nguvu ya kuomba kazi tena kwenye timu hiyo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.