TIMU ya Tanzania ya Wanawake, Kilimanjaro Queens leo Desemba 9 imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Eritrea kwenye michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Chalenji) inayofanyika nchini Uganda.
Mchezo huu uliochezwa uwanja wa Njeru-Jinja mchezaji wa Tanzania, Joyce Meshack alisepa na mpira.
Aisha Masaka alifunga mabao mawili na alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 21 bao la pili alifunga dakika ya 41.
Mabao matatu ya Joyce Meshack yalifungwa dakika ya 29, 54, 62 na kuifanya Tanzania kushinda mchezo wake wa leo.
Post a Comment