KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa wachezaji wake wanajuhudi uwanjani jambo linalowapa mafanikio.
Manchester United imeanza kuleta matumaini kwenye Ligi Kuu England baada ya kushinda mechi mbili kubwa mfululizo baada ya kuichapa Tottenham Hotspur mabao 2-1 na Manchester City mabao 2-1.
Ole amesema kuwa wachezaji wake wanahitaji mafanikio anaamini watakuwa bora muda wote kwani amekuwa akiwapa mbinu ambazo zinawakuza uwezo wao pamoja na jitihada zao binafsi.
Msimu huu Manchester United imezitungua timu kubwa ikiwa ni pamoja na Chelsea, Leicester City, Tottenham Manchester City ililazimisha sare mbele ya vinara Liverpool na Aston Villa.
United ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi zake 24 baada ya kucheza mechi 16 ikiwa tofauti na pointi 22 na vinara Liverpool.
Post a Comment