BEKI kisiki wa Yanga Lamine Moro inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na Simba ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho kwenye usajili wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 16.

Moro amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Yanga kwa kuokoa michomo ya hatari jambo ambalo Simba inaelezwa kuwa anaweza kuwafaa baada ya kuonekana anacheza mithili ya Kelvin Yondani.

Habari ziaeleza kuwa tayari Moro raia wa Ghana yupo kwenye mazungumzo na mabosi wa Simba ambao waliwahi kumleta Bongo kufanya nae majaribio ila waliachana nae kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na nafasi ndani ya kikosi cha Simba.

Moro kwa sasa yupo ndani ya Yanga na ameandika barua kuomba malipo yake ambayo hajalipwa ndani ya kikosi cha Yanga.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.