Dar es Salaam.Kaimu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Mwina Kaduguda amesema katika uongozi wake kipaombele chake ni kuhakikisha anaimarisha uchumi wa klabu.
Kaduguda anayekaimu nafasi hiyo baada ya Swedy Mkwabi kujiuzulu amesema moja ya mipango yake ni kumshauri Mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji (Mo), ili matawi ya klabu hiyo kuwa masoko ya bidhaa za Simba.
Kaduguda amesema mpango uliopo sasa ni kuhakiki matawi yote ya klabu na watayageuza kama vikundi vya ujasiriamali wakikopeshwa mitaji na mwekezaji wao.
"Mpira ni pesa, huwezi kufanikiwa kwa kutaka ubingwa wa Afrika wakati timu ina njaa, lakini katika uongozi wangu si klabu tu tunahitaji iwe na uchumi mzuri, hata wanachama wetu kupitia kwenye matawi yao ambako kama nilivyosema, tutayafanya matawi hayo kuwa masoko ya bidhaa za klabu," alisema.
Kiongozi huyo wa Simba alitolea mfano uchumi wa klabu kwa sasa na miaka ya nyuma akidai, enzi za nyuma timu hiyo ilikuwa ikilala kwenye viti uwanja wa ndege ikisubiri kubadili ndege, lakini sasa tabu hizo hazipo.
"Nakumbuka kuna mwaka tumelala uwanja wa ndege, wachezaji wakijifunika makoti kwenye viti vya uwanja wa ndege wa Afrika Kusini tukielekea katika Ligi ya Mabingwa, kwa kuwa tulikosa fedha ya kuwalaza wachezaji wetu hotelini.
"Sasa pesa ipo, tangu ujio wa Mo haijawahi kutokea, kilichopo sasa ni kuendelea kumpa sapoti na kuipa sapoti klabu, ushirikiano ndiyo kitu kikubwa katika mafanikio ya Simba," alisema Kaduguda akishangiliwa kwa nguvu na wanachama

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.