Klabu ya soka ya Afc Arusha imetangaza kifo cha Kocha Msaidizi wa klabu hiyo Luke Juma kilichotokea hapo Jana.
Habari iliyotolewa leo kwa vyombo vya Habari na Ofisa Habari wa klabu hiyo Bahati Msilu imeeleza kuwa Luke amefundisha AFC Arusha kwa nyakati tofauti akiwa ni kocha mpaka umauti unamkuta Luke alikuwa ni kocha Msaidizi wa klabu ya AFC Arusha akishirikiana na Mwalimu Ulimboka Mwakingwe.
Klabu ya AFC inatoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu jamaa Na marafiki wote na Familia ya wapenda michezo wote hapa nchini
Post a Comment