KWA sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Inatarajiwa hali kuwa shwari hivi karibuni kutokana na dua za familia ya wanamichezo kwa Mungu pamoja na imani za wengi kwani hakua lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho.
Msimu utakaporejea na kumalizika kwa mwaka 2019/20 wapo wachezaji ambao muda wao wa kuishi ndani ya klab zao kwa sasa utakuwa umemuguka hivo iwapo timu inahitaji saini za nyota hao ni rahisi kuwapata.
Hili hapa kosi ambalo mikataba yao inameguka mwishoni mwa msimu
1. Razack Abarola yupo zake Azam FC
2. William Luccian 'Gallas' wa Polisi Tanzania.
3. Andrew Vincent, 'Dante' wa Yanga.
4. Pascal Wawa wa Simba.
5.idd Mobby wa Polisi Tanzania.
6. Mzamiru Yassin wa Simba.
7. Shiboub Sharaf wa Simba.
8. Hassan Dilunga wa Simba.
9. Marcel Kaheza wa Polisi Tanzania.
10. Relliats Lusajo wa Namungo.
11. Sixtus Sabilo wa Polisi Tanzania.
Post a Comment