ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC ameshikilia mkataba wa nyota wa timu hiyo Donald Ngoma.

Cioaba raia wa Romania kwa sasa yupo zake likizo baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Tayari nyota wa timu hiyo, Obrey Chirwa ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja na atakuwepo pia msimu ujao akiwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza.

Habari zinaeleza kuwa Chirwa ni pendekezo la Cioaba hivyo hata hatma ya Ngoma ipo mikononi mwake.

"Chirwa ameshamwaga wino baada ya kocha kupendekeza, kuhusu Ngoma pia ni yeye ambaye ataamua asepe ama abaki," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa bado Ngoma ni mchezaji wa Azam FC likitokea jambo mambo yatakuwa wazi.

Msimu huu Azam FC ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 54 Ngoma ametupia mabao mawili kati ya 37 baada ya kucheza mechi 28 za ligi.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.