Ndani ya siku 10 Uingereza imepoteza takribani watu 4,000 kwa vifo kutokana na ugonjwa wa Corona na inazua hofu ya kurejea kwa EPL kwa ajili ya kumalizia msimu.
Taarifa zinaeleza waliofariki dunia ni 3,811 kwa wale walio hospitali na waliokuwa wakijiugiza makwao na hii ni ndani ya siku 10 tu.
Hata hivyo kuna taarifa kwamba ni zaidi ya watu 6,000 kwa kuwa wengine hawakuwa wamejiandikisha hospitali na wamekuwa wakijiuguza majumbani.
Hii maana yake bado kunakuwa na hofu katika suala la kurejea kwa Ligi Kuu England.
Tayari baadhi ya timu na Arsenal ikiwa ya kwanza zilirejea mazoezini.
Hata hivyo, kuendelea kuongezeka kwa vifo huku Uingereza ikiwa haina mgonjwa aliyepona inazidi kuamsha hofu kama kutakuwa na nafasi ya kurejea kwa ligi hiyo ili kumalizia msimu.
Idadi hiyo ya vifo kutokea Aprili 10 hadi 24 pekee inaonekana kuwa kubwa na inatisha.
Bado kuna mjadala mkubwa kuhusiana na kurejea kwa EPL ambayo inatakiwa kuwa inachezwa bila ya mashabiki.
Post a Comment