PAUL Nonga, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Lipuli FC chenye maskani yake mkoani Iringa anawapa tabu mabosi wake hao kwa sasa kumtafuta mbadala wake.

Nonga ameliambia Championi Ijumaa kuwa tayari amewajulisha viongozi wake kuanza kutafuta mbadala wake pale mkataba wake utakapomalizika Juni Mosi, 2020 kwa kuwa anahitaji changamoto mpya.

Championi Ijumaa lilimtafuta Ofisa Habari wa Lipuli FC, Clement Sanga ili azungumzie harakati za kumtafuta mbadala wa Nonga ambapo alisema kwa ufupi: “Kwa sasa nipo bize kushughulikia hayo mambo,".

Nonga ambaye anavaa kitambaa cha unahodha msimu huu wa 2019/20 ametupia mabao 11 na kutoa pasi nne za mabao jambo linalowapasua Lipuli kumpata mbadala wake

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.