MARCEL Kaheza, mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa ndoto zake ni kuwa mchezaji wa kimataifa baada ya miaka mitano hapo mbele.

Kaheza mwenye mabao saba na pasi tano ndani ya Polisi Tanzania leo ni kumbukizi yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka kadhaa.

Anapenda kuvaa jezi namba 10 mgongoni alivutwa ndani ya Simba akitokea klabu ya Majimaji ya Songea ambayo inapambana ndani ya Ligi Daraja la Kwanza na kwa sasa maisha yake ndani ya Polisi Tanzania yupo kwa mkopo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema:"Ninamshukuru Mungu kwa ulinzi wake na upendo pia, kikubwa ambacho ninakifikiria baada ya miaka mitano niweze kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

"Hiyo itanipa nguvu ya kupambana kwa ajili ya taifa pamoja na pale ambapo nitakuwa ninacheza,, kikubwa ni sapoti na kufanya kazi kwa juhudi," .

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.