WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe ameitaka Klabu ya Pamba SC kujikita katika uwekezaji wa timu za vijana ambao watakuwa na faida kwa taifa.

Mwakyembe ameyasema hayo baada ya Klabu ya Pamba kumtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.

 "Nawaomba sana Klabu ya Pamba muwekeze kwenye vituo vya  vijana ili mzalishe vijana kwa wingi kwakua ndio silaha ya taifa katika soka la nchi yetu ukiangalia Serikali kila mwaka hutumia zaidi ya bilioni tatu kuendesha mashindano ya Umiseta na Umitashumta ili kuibua vipaji,“ alisema Mwakyembe.

Kaimu Mwenyekiti wa Pamba, Aleem Alibhai alimuahidi Waziri Mwakyembe kwamba atahakikisha timu hiyo inaanzishwa haraka iwezekanavyo.

"Pamba  haikuwa na timu ya vijana isipokuwa iliingia makubaliano na kituo cha kukuza vipaji cha Pamoja Sports Academy ambacho kiko mwanza kwa ajili ya kuzalisha vijana, lakini sasa na sisi tutajipanga,” alisema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.