TARIQ Seif, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa atahakikisha anaendelea kutupia kila anapopopata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Seif ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo alisajiliwa mwezi Januari akitokea nchini Misri na mechi yake ya kwanza ilikuwa mbele ya Biashara United ambapo alitupia bao lake la kwanza.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimesambaa duniani kote.
Seif amesema:-"Nitahakikisha naendelea kufanya vizuri na kufunga kwa kila mchezo ambao nitakuwa napata nafasi ili kuendeleza rekodi yangu ya ufungaji na niweze kuisaidia timu yangu kwenye mashindano yeyote ambayo tutapata nafasi ya kushiriki.
Kwenye Ligi Kuu Bara jumla Sei ametupia mabao matatu ambapo Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 na imetupia mabao 31
Post a Comment