SERIKALI ya Ufaransa imezuia kuendelea kwa michezo hadi Septemba mwaka huu, huku Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edouard Philippe, akisema msimu wa 2019-20 umekwisha.

Awali matumaini ya Chama cha Soka Ufaransa ilikuwa ni kwamba ligi zao zitaendelea Juni 17 na msimu kumalizika Julai 25 baada ya ligi kusitishwa Machi 13, mwaka huu kutokana na janga la corona.

Kauli ya Serikali inamaanisha kwamba, Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’ kwa msimu huu ndiyo basi tena.

Mpaka sasa, bado haijaeleweka Chama cha Soka Ufaransa itaamua kutoshusha timu au kupandisha au kuangalia msimamo ulivyo.

Mabingwa watetezi wa Ligue 1, Paris St-Germain, wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 12 mbele ya Marseille, huku zikiwa zimesalia mechi kumi.

Toulouse wapo mkiani wakiwa na pointi 17, juu yao wapo Amiens waliowaacha kwa pointi kumi. Nimes ni wa 18

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.