Maisha YAMEBADILIKA kabisa, Ile jana yetu tulivyozoea si leo tunayoishi lakini hakuna ujanja yote ni maisha na lazima tuendelee kuishi.


Kitu kikubwa sana nawasihi tujiyambue na kujua ugonjwa huu ni hatari, Corona si utani wala sinema, ipo na tayari ipi mitaani kwetu... Waungwana CHUKUA Tahadhari wakati ukiendelea na maisha.

Mambo ya kusema unasubiri kuambiwa au kuwekeza nguvu nyingi ukisubiri KULAUMU ni kujiumiza mwenyewe.

Angalia Corona tayari imeonyesha HAIJALI rangi, kabila, ukubwa wa mwili, cheo wala umaarufu na mifano rundo tunayo... Wewe na mimi ni KINA NANI HASA tusalimike wakati TUKIFANYA MZAHA... Chukua hatua sasa acha kulala kwa makusudi baadaye uanze kulaumu kwa kuwa kama una macho TAYARI UMEONA na kama una masikio TAYARI UMESIKIA... #staysafe

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.