KUHUSU Nadir, Jembe anaandika hivi:-

KWELI muda umekwisha mwanangu Nadir, unakuwa hauna ujanja lakini kama ungekuwa unaruhusu, ningekushauri urudi tena na kuitumikia Yanga au Tanzania yetu.

Umeondoka na utamu wako, very pro, muda umeisha wala hukusumbua ukakaa zako kando. Najua watu wa mpira wepesi sana kusahau, wengi wameisha kusahau, siku hizi zaidi wanamzungumza Lamine Moro, wana haki ndio wakati wake.

Mimi, kamwe siwezi kukusahau, mwanangu chuma, beki usiye na mambo mengi ya sifa lakini mambo mengi ya manufaa.

Naikumbuka penalti yako dhidi ya Al Ahly, ninaamini hadi leo kipa wao anaiota. Bahati mbaya Bahanuzi alishindwa kumalizia kazi (mambo ya mpira). Nakumbuka namna ulivyowatuliza Eto’o na wenzake, nakumbuka ulivyomtwaga Drogba buti la uso na baada ya mechi akakusifia.


Nakumbuka mengi sana na bado nakumbuka mwaka tuliokutana Rwanda, Yanga wakataka kukusajili kwa mara ya kwanza. Namna ulivyoiongoza Zanzibar kuitwanga Rwanda mbele ya Rais Kagame.

Hata kama ni mstaafu, katika moyo wangu wa wachezaji ninaowathamini sana kutokana na namna walivyoutendea haki mpira wa Tanzania pamoja na yote, bado utabaki moyoni mangi kuwa wewe ni LEGEND na hadithi ndefu zaidi ya kitabu.

Nakupa hongera zaidi, Mungu akupe umri zaidi kwa kuwa unapenda wengine waendelee, ninaamini utaendelea kuwa msaada mkubwa sanaaa

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.