YIKPE Gnamien, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa akipewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza pale Ligi Kuu Bara itakaporejea atafanya mambo makubwa kwenye timu yake.

Gnamien ambaye ni ingizo jipya alijiunga na Yanga msimu huu kwenye dirisha dogo akitokea Klabu ya Gor Mahia ambapo alivunja mkataba wake kwenye timu hiyo.

Ndani ya ligi alifunga bao kwenye mechi yake dhidi ya Singida United uliochezwa Uwanja wa Namfua.

Nyota huyo amesema:"Nipo ndani ya Yanga na kwa sasa ninaendelea kuchukua tahadhari kwa ajili ya kujilinda na Virusi vya Corona ili ligi itakaporejea niwe kwenye ubora.

"Nina amini nafasi ya kufanya vizuri ipo kutokana na uwezo wangu hivyo mashabiki ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari ili hali ikiwa shwari tuwe pamoja," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.