DARUES Saliboko, mshambuliaji wa Lipuli amesema kuwa kikosi cha Yanga kinamhitaji mshambuliaji kama yeye ili akatulize eneo la katikati ambalo anaamini huwa linakosa utulivu.

Saliboko anayetupia jezi namba 10 mgongoni amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya Lipuli akiwa ametupia mabao nane ambapo habari zinaeleza kuwa yupo kwenye rada za Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema:"Yanga ni timu kubwa na imara nina amini kinachokosekana pale katikati ni mtu wa kuwatuliza ili wafanye makubwa na iwapo nikaingia pale nitafanya kazi yangu kwa umakini.

"Kingine kinachotakiwa kwa timu kama Yanga ni umakini mkubwa wa wachezaji kwani kila mechi inakuwa na presha kubwa jambo linalowafanya waonekanae kushindwa kufanya kama ilivyokuwa zamani licha ya kuwa ni timu kubwa na yenye nguvu,".

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 27 kibindoni ina pointi 51 na imetupia mabao 31 na kinara wao wa utupiaji ni David Molinga mwenye mabao nane

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.