SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba amesema kuwa kwa wakati huu wa maambukizi ya Virusi vya Corona ni lazima kila mmoja akachukua tahadhari kwani hali bado haijawa shwari.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa ili hali iwe shwari ni muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari kwa ajili ya afya yake na ya mwenzake pia.
"Wapo watu ambao bado wanachukulia suala hili katika hali ya kawaida jambo ambalo halipendezi, tunaoana kwamba Serikali inazidi kupambana ili kuweka mambo sawa ila wapo wengine kwa makusudi tu wanaamua kuendelea na mambo yao.
"Haina maana kwamba hawapaswi kuendelea na mambo yao hapana kitu cha msingi ni kuzingatia kwanza usalama wao na kufuata maelekezo ya Serikali yanayotolewa kila mara pamoja na yale ya Wizara ya afya," amesema
Post a Comment