BEKI kiraka wa Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa kwa sasa amekuwa akitumia muda mwingi nyumbani tofauti na mwanzo ambapo alikuwa bize na kibarua chake cha kucheza ndani ya Simba.
Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia jambo lililofanya wachezaji wengi kuwa majumbani wakichukua tahadhari na kufanya mazoezi binafsi.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nyoni amesema kuwa akiwa nyumbani ni mwendo wa barakoa pamoja na kuwa balozi kuhusu Virusi vya Corona.
“Kwa sasa natumia muda mwingi kuwa nyumbani huku nikichukua tahadhari dhidi ya Corona pia nimekuwa ni balozi wa hiyari katika kupambana na maambukizi dhidi ya Virusi vya Corona.
“Tunachuka tahadhari pamoja na familia kwani kila muda tumekuwa tukinawa mikono na kuendeleza ule utamaduni wetu wa zamani ila kwa sasa ni balaa, ninapenda kuona na wengine pia wakichukua tahadhari ili hali ikiwa shwari tuendelee na shughuli zetu,” amesema.
Kwenye Ligi Kuu Bara licha ya kuwa ni beki, Simba ikiwa imefunga mabao 63 yeye ana bao moja alilowatungua mabosi wake wa zamani Azam FC Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda kwa mabao 3-2
Post a Comment