YUSUPH Mhilu mshambuliaji anayekipiga ndani ya Kagera Sugar, amesema kuwa moja ya mabeki anaokubali uwezo wao ndani ya Bongo ni pamoja na Kelvin Yondani anayekipiga Yanga.
Mhilu ambaye aliwahi kucheza ndani ya Yanga pamoja na beki huyo, amesema kuwa miongoni mwa wabeki wazawa ambao wanafanya kazi zao kwa umakini muda wote jina la Yondani haliwezi kukosekana.
Mhilu alisema kuwa alipopata bahati ya kuifunga Yanga walipokutana Uwanja wa Uhuru jijini Dar mbele ya Yondani, alijipongeza kwa kitendo chake cha kishujaa.
“Kazi ya mshambuliaji huwa haitazami kama aliwahi kuitumikia timu fulani basi aionee huruma, hapana, yeye ni kufunga tu, nilipofunga mbele ya Yondani nilijipongeza kwani sio kazi rahisi kupita mbele ya beki yule.
“Kwa muda wote ambao nimekuwa nikicheza mpira, Yondani ni miongoni mwa mabeki bora ambao wanatambua majukumu yao uwanjani, kwa hilo anastahili pongezi kwani mchango wake ni mkubwa hata kwenye taifa pia,” alisema Mhilu
Post a Comment