BAADHI ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshauri Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kuifuta ligi msimu huu na ubingwa kuipa Simba ambayo inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi nyingi zaidi ya timu zinazofuatia wakidai hali siyo salama kwa ligi kurejea kwa sasa. 

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja katika kikao cha bunge juzi Alhamisi, ambapo kwa pamoja waliitaka TFF kufikiria kwa kina juu ya kuifuta ligi hiyo kutokana na janga la Corona, huku wakisema timu mbili za juu ziende kuiwakilisha nchi kimataifa.


Akitoa maoni yake juu ya mwenendo wa ligi kuu nchini, Nkamia alisema: - “Nawaomba TFF, waangalie uwezekano wa kuifuta ligi na timu mbili za juu mmoja akipewa ubingwa na mwingine akipewa tiketi ya kwenda kushiriki mashindano ya FA, kwa sababu hali ya sasa siyo salama kwa ligi hiyo kuendelea kutokana na janga la Corona ni vyema wakatumia busara hiyo

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.