STRAIKA wa Barcelona, Martin Braithwaite amesema anataka kukaa ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi ya mkataba ambao anao kwa sasa kwa kuhakikisha ainafanya klabu hiyo kuwa bora zaidi.
Braithwaite amejiunga na Barcelona akitokea Leganes katika usajili wa dharura msimu huu hii ni baada ya Barca mastaa wake Luis Suarez na Ousmane Dembele kutupwa nje kutokana na majeruhi.
Straika huyo ameingia mkataba na Barcelona ambao utadumu mpaka mwaka 2024 kuitumikia klabu hiyo.
Straika huyo amesema: “Ninahakika kuwa nitakaa hapa Barcelona kwa muda mrefu zaidi ya hata mkataba wangu.
“Nataka kuwa kucheza na kutwaa makombe sababu ni malengo yetu na kuja hapa ni wakati wangu muafaka mimi kuweka biidi na kuwa msaada.
“ Hapa naangalia wale malegendari walifanya nini katika klabu kuangalia yale mazuri ambao walifanya na kuacha alama katika klabu ndiyo kitu kizuri ambacho hata mimi hapa tajifunza kupitia kwa kwa kuhakikisha na weka alama hapa Barca hata vizazi vijavyo vijekuona kitu ambacho nilifanya nini hapa,”alisema.
Straika huyo tangu ajiunge na klabu hiyo amecheza mechi tatu za La Liga kabla ya kusimama kutokana na virusi vya corona amecheza dhidi ya Eibar, Real Madrid na Real Sociedad
Post a Comment