STAA wa Klabu ya Inter Milan, Alexis Sanchez wiki hii anatarajiwa kurejea jijini Milan akitokea  nchini kwao Chile  baada ya kupewa ruhusu licha ya Serie A kupigwa stop.
 Sanchez alienda Chile kutokana na kuwa na matatizo binafsi ya kifamilia hivyo uongozi wa klabu ulimpatia ruhusu licha ya wachezaji wengine kusalia Italia wakiwa karantini kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona.
Sanchez kwa sasa anakipiga katika klabu hiyo, kwa mkopo akitokea katika klabu ya Manchester United ya Ligi Kuu ya England.
 Straika huyo aliruhusiwa na uongozi kwenda Chile, lakini aliongezewa muda zaidi wa kusalia huko kutokana na hali  mbaya ya Virusi vya Corona nchini Italia.
 Taarifa kutoka Italia zimeeleza kuwa staa huyo baada ya kutua nchini humo kabla ya kuingia mtaana atatakiwa kukaa karantine kwa siku 14 ili kuangalia afya yake.

 Hata  hivyo kwa upande mwingine imeelezwa kuwa staa huyu kuelekea msimu ujao, Klabu ya Inter Milan haina mpango wa kuendelea naye hivyo anarejea katika klabu yake ya Man United na hii ni kutokana na kuwa na mshahara mkubwa.
 Kwa msimu huu ndani ya Serie A amecheza mechi 15 sawa na dakika 596  katika michuano yote na hii ni kutokana na kuwa nje kwa muda mrefu kuuguza majeraha.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.