RAMADHAN Kabwili, mlinda mlango namba tatu wa Yanga amesema kuwa kinachomkosesha namba ndani ya kikosi hicho ni ushindani wa namba pamoja na chaguo la mwalimu.
Kabwili msimu huu Kwenye mechi za Ligi Kuu Bara hajakaa Langoni ambapo Yanga ikiwa imecheza mechi 27 zaidi ya kuisha benchi.
Alipata nafasi ya kuonyesha uwezo wake visiwani Zanzibar Kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Kabwili amesema:"Ushindani wa namba umekuwa mkubwa na kila kipa ana uwezo wake jambo ambalo linanifanya nisipate nafasi ya kuanza ila bado nipo Yanga. "Mwalimu pia ana chaguo lake, nilipata nafasi ya kuanza Kwenye kombe la Mapinduzi na kwa sasa bado napambana ili kuwa bora,".
Post a Comment