ADAM Salamba nyota wa Tanzania anayekipiga ndani ya Klabu ya Al-Jahra SC, iliyopo Barani Asia amesema kuwa kikubwa kwa sasa ni kila mmoja kuomba ili janga hili la Virusi vya Corna lipite.
Akizungumza na Saelh Jembe, Salamba amesema kuwa janga hili ni la dunia hivyo ni lazima kila mmoja akaongeza juhudi za kuomba na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
“Huku tumeshindwa kuendelea na shuguli zetu za kila siku kutokana na Virusi vya Corona hivyo ni muhimu kila mmoja kuendelea kufanya dua ili Mungu atuepushe katika hili ili lipite salama,” amesema Salamba
Post a Comment