RELLIATS Lusajo nahodha anayekipiga ndani ya Klabu ya Namungo ameziingiza vitani timu kubwa tatu ambazo ambazo ni Simba, Yanga na Azam zinazopambana kuipata saini yake kwa ajili ya msimu ujao.
Lusajo amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ni miongoni mwa wazawa wenye mabao mengi akiwa ni namba moja ndani ya Namungo, jambo linalowavutia mabosi wengi wa timu hizo.
Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eyamel inaelezwa kuwa ina nia ya kumsaka mshambuliaji baada ya David Molinga kushindwa kuonyesha makeke ambayo waliyatarajia kwani mpaka sasa amefunga mabao nane pekee.
Azam na Simba pia wapo kwenye mpango wa kusuka vikosi vyao upya ambapo hesabu zao pia zinamhusu Lusajo mwenye mabao 11 na pasi tatu za mabao.
Lusajo amesema kuwa:"Kuwa mchezaji ni jambo ambalo ninalipenda na ni kazi yangu, ninajiamini katika uwezo wangu ninaweza kucheza popote," ,
Post a Comment