MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa mabeki wengi wamekuwa wakimkamia uwanjani jambo ambalo linamfanya awe makini muda mwingi akiwa ndani ya uwanja.

Kagere mwenye mabao 19 ndani ya Ligi Kuu Bara amekuwa kwenye mwendelezo wa ubora wake ambapo msimu uliopita alifunga mabao 23 na kumaliza akiwa kinara kwa mwaka wa 2018/19.

Kagere amesema:"Nikiwa uwanjani mabeki huwa wananikamia kwa kunikaba kwa kutumia nguvu nyingi jambo ambalo limenifanya niwe makini nikiwa uwanja.

"Kazi yangu ni kufunga hasa kwa nafasi yangu ninajitahidi kuona namna gani ninaweza kufikia malengo yangu na ya timu ndani ya uwanja," .

Mbali na kufunga Kagere pia ametoa pasi tano za mabao ambapo Simba imefunga mabao 63, kwa sasa ligi imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.