ARSENAL imeamua kujiweka kando kwenye ishu ya mazungumzo ya kuongeza mkataba na nyota wao Pierre-Emerick Aubameyang.
Inaelezwa kuwa huenda nyota huyo mwenye miaka 30 akaibukia ndani ya Klabu ya Inter Milan ambayo inaiwinda saini yake.
Auba ambaye ni nahodha wa Arsenal inaelezwa kuwa alikuwa anataka kuongezewa mkwanja wa malipo jambo ambalo limekuwa gumu kupenya kwenye maskio ya mabosi hao.
Miongoni mwa klabu ambazo zinatajwa kuwinda saini yake ni pamoja na Barcelona na Manchester United
Post a Comment