INAELEZWA kuwa mabosi wa Simba wanaiwinda saini ya nyota wa Yanga, David Molinga ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao kwa sasa.
Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa ya Simba kuiwinda saini ya Molinga ni uwezo wake wa kutupia mabao pamoja na kupiga faulo za moja kwa moja.
Ndani ya Yanga Molinga amefunga mabao nane ambapo mawili alifunga kwa faulo iliyojaa nyavuni huku bao moja akifunga kwa penalti.
"Mabosi wa Simba wanaitaka saini ya Molinga wanaamini ana uwezo mkubwa wa kufunga kutokana na kuwa kinara wa kutupia mabao kwa sasa.
"Licha ya wengi kujiuliza kwa nini ni Molinga swali la msingi ni kuuliza nani kinara wa kutupia ndani ya Yanga? Ikiwa amefunga mabao hayo na amekuwa akisugua benchi nini kitatokea akitumia muda mwingi uwanjani," ilieleza taarifa hiyo.
Chanzo: Championi
Post a Comment