Beki wa kushoto Mohamed Hussein Zimbwe, ’Tshabalala’ nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa mbali na kuchukua tahadhari kwa wakati huu wa maambukizi ya Virusi vya Corona anatumia muda wake pia kucheza gemu.
Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kutokana na tamko la Serikali, Machi 17 lililotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya mgonjwa wa kwanza wa Corona kupatikana hapa nchini.
Akizungumza, Zimbwe amesema kuwa anatumia muda wake kushinda nyumbani pamoja na kucheza gemu.
“Nipo nyumbani kwa sasa ninachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na ninapata muda pia wa kucheza gemu kwani ni miongoni mwa vitu ninavyopenda,” alisema Zimbwe.
Zimbwe, amehusika kwenye mabao manne yaliyofungwa na Simba msimu huu.
Post a Comment