DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa amekumbuka kurudi uwanjani kucheza ila anashindwa kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nchimbi amesema kuwa katika vitu ambavyo amevikumbuka kwa sasa ni kurudi uwanjani kucheza pamoja na makelele ya mashabiki uwanjani.

"Nimekumbuka kurudi uwanjani na kucheza mpira lakini inakuwa ngumu kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

"Dua yangu ni kuona kwamba hili linapita na maisha yetu yarudi kwani kuna vingi tunavikosa na hili janga sio mchezo, zile kelele za mashabiki pia kwa sasa inakuwa ngumu kuziskia," amesema.

Nchimbi ametupa mabao sita ndani ya ligi ambapo mawili alitupia akiwa Yanga na manne alitupia akiwa Polisi Tanzania

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.