KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroec amesema kuwa hana tatizo na kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu na anaamini anaweza kuwa bora baadaye ikiwa ataongeza juhudi kwenye mazoezi.
Ajibu ni ingizo jipya msimu huu ndani ya Simba alijiunga nayo kwenye usajili wa dirisha kubwa akitokea Klabu ya Yanga ambayo alicheza misimu miwili akitokea Simba.
Sven amesema:-"Ni mchezaji mzuri na anauwezo mkubwa kwani kuna mechi nilikuwa ninampa nafasi na alikuwa anatimiza majukumu yake vizuri sina tatizo naye kabisa.
"Kikubwa nimekuwa nikimwambia afanye mazoezi kwa juhudi ili kuzidi kuwa bora," amesema.
Ajibu amefunga bao moja ndani ya Simba na kutoa pasi nne za mabao akitumia mguu wake wa kulia huku Simba ikiwa imefunga mabao 63.
Post a Comment