UONGOZI wa Mbeya City umesema kuwa unaendelea kuomba dua usiku na mchana hali ikae shwari ili maisha yaendelee kama zamani.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja amesema kuwa wanashindwa kuendelea na program za kawaida kutokana na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.
"Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona tumeshindwa kuendelea na program ambazo zilikuwa zimepangwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chetu hivyo kwa sasa kila mmoja yupo majumbani kwake.
"Maombi yetu ni kuona kwamba mambo yanakuwa salama kisha mambo yakaendelea kama zamani kwani tayari tulikuwa tumeanza kuwa kwenye ubora," amesema.
Mbeya City ipo nafasi ya 17 kibindoni ina pointi 30 baada ya kucheza mechi 29
Post a Comment