ALVARO Morata, mshambuliaji wa Klabu ya Atletico Madrid amesema kuwa kukabiliana na beki kitasa wa Liverpool, Virgil van Dijk kunahitaji akili kwani ni ngumu mithili ya kupanda mlima.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa kupenya kwenye himaya ya beki huyo ni jambo la kujivunia kutokana na umakini wake.



Nyota huyo mwenye miaka 27 alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda mabao 4-2 dhidi ya Liverpool ambao ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Amewataja mabeki wengine visiki kukabiliana nao ambao ni Sergio Ramos wa Real Madrid na Giorgio Chiellini wa Juventus.


Staa huyo yupo kwa mkopo ndani ya Atletico Madrid akitokea Chelsea ambapo amecheza jumla ya mechi 38 na kutupia mabao 14

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.