PAUL Nonga, mshambuliaji wa kikosi cha Lipuli ambaye alikuwa miongoni mwa kikosi cha Mbeya City kilichotamba msimu wa 2013/14 ndani ya Ligi Kuu Bara amesema kuwa nidhamu iliwabeba.

Kwa sasa kikosi cha Mbeya City kinapambana kutetea nafasi yake ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo hakikuwa na mwendo mzuri kabla ya ligi kusimamishwa msimu huu kutokana na Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa wakati ule kila mmoja alikuwa anatimiza majukumu yake kwa wakati na kujituma mwanzo mwisho.

"Wakati ule tulikuwa makini katika kutimiza majukumu ambayo tumepewa na kufanya kwa wakati, kikubwa kilichokuwa kinatubeba ilikuwa ni ushirikiano wetu.

"Nguvu ya mashabiki na ushirikiano ni miongoni mwa vitu ambavyo tulikuwa tunavifanya kila wakati mpira unahitaji nidhamu," amesema.

Kwa sasa Mbeya City ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 29.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.