BIGIRIMANA Blaise nyota wa timu ya Namungo amesema kuwa ndoto yake ni kuona anaweza kucheza ndani ya timu kubwa Bongo ikiwa ni pamoja na Yanga, Azam na Simba.

Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa mwiba ndani ya ligi kwa kucheka na nyavu ni miongoni mwa washambuliaji walio ndani ya tano bora kwa kutupia akiwa na mabao 10.

Akizungumza na Saleh Jembe, Blaise amesema kuwa hana mashaka na uwezo wake kwa sasa yupo tayari kukipiga ndani ya Bongo kwenye timu kubwa iwapo zitafuata utaratibu.

"Nipo na mkataba na Namungo kwa sasa ila ikiwa itatokea klabu kubwa Bongo zikahitaji saini yangu ni suala la kuzungumza ili kuona namna gani tutamalizana nao.

"Kazi ya mchezaji ni kucheza bila kuchagua aina ya timu anayokwenda hivyo ikitokea nitacheza bila tatizo kwani mkataba wangu upo mbioni kumeguka," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.