WAZIR Jr, mshambuliaji namba moja ndani ya Mbao FC amesema kuwa iwapo timu yake itashuka daraja nafasi yake ya kubaki klabuni hapo itakuwa ndogo anaweza kusepa.

Jr amesema kua dua kubwa ni kuona kwamba timu hiyo haishuki daraja hivyo pindi Ligi Kuu Bara itakaporejea watapambana kufa na kupona kupata matokeo chanya kwenye mechi zilizobaki.

Kwa sasa ligi imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wakati inasimama Mbao FC yenye maskani yake Mwanza ilikuwa nafasi ya 19 ikiwa imefunga mabao 19 huku Jr akifunga mabao saba na pasi mbili za mabao baada ya kucheza mechi 29 kibindoni ina pointi 23

"Ni ngumu kwangu kubaki iwapo timu itashuka daraja lakini hiyo siyo hesabu yangu kubwa kwa sasa, muda huu ni wakati wa dua kwanza hali irejee kwenye ubora wake na maisha ya soka yaendelee.

"Imani yangu ni kwamba bado tuna nafasi ya kubaki ndani ya ligi hilo lipo wazi, wachezaji tumekubaliana kupambana na kufanya kazi kwa kushirikiana ili tuwe katika malengo ambayo tumejiwekea," .

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.