UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauwezi kushindwa kupata saini yoyote ya mchezaji anayekipiga ndani ya timu za Bongo kwa sasa kutokana na kujipanga kiuhakika.

Kauli hiyo ya kishujaa ni salamu kwa mabosi wa Yanga ambao ni GSM walio kwenye mpango wa kujenga kikosi matata cha Yanga msimu ujao huku ikielezwa kuwa wamekutana chimbo la beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto.

Mkurugenzi Mtendaji wa Simba, Senso Mazingiza amesema kuwa hawana mashaka iwapo kocha Sven atapendekeza jina la mchezaji amwage wino ndani ya Simba.

"Ikiwa kocha atapendekeza jina la mchezaji kusajiliwa Simba haiwezi kuwa na shida tupo vizuri hasa kwa wachezaji wa ndani hakuna kinachoshindikana,".

Dau la Mwamnyeto linatajwa kuwa ni milioni 100 huku Yanga inaelezwa kuwa tayari wameanza mazungumzo na uongozi wa Coastal Union ili kuipata saini ya beki huyo chipukizi.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.