ABDULHALIM Humud ‘Gaucho’ kiungo anayekipiga ndani ya Mtibwa Sugar amepata kigugumizi ghafla kuzungumzia dili lake la kuwindwa na Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Luc Eymael.

Gaucho amekuwa kwenye ubora wake msimu huu akiwa ndani ya Mtibwa Sugar ambapo alikuwa miongoni mwa wachezaji walionyanyua makwapa kutwaa taji la Mapinduzi baada ya kuitungua Simba bao 1-0.

Gaucho amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia dili lake la kujiunga na Yanga kutokana na kuwa mali ya Mtibwa Sugar.

“Kwa sasa siwezi kuzungumzia ishu ya saini yangu kuhitajika na Yanga kutokana na kuwa ni mali ya Mtibwa ila wakati ukifika nitaweka wazi.

“Bado ninaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwa sasa na ninafanya mazoezi binafsi ili kuwa bora kwani kuna program ambazo tumepewa,” amesema Humud.

Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake kibindoni 33, Humud ametupia mabao mawili kati ya 22 ya timu hiyo

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.