OBREY Chirwa, mshambuliaji wa Azam FC ameongeza kandarasi ya mwaka kuendelea kuitumikia Azam FC huku ikitajwa kuwa sababu kubwa ni kuthamini mchango wa nyota huyo kikosi hapo.

Mkataba wa Chirwa ulikuwa unameguka mwisho wa msimu huu na alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za mabosi wake wa zamani Yanga ambao walikuwa wanahitaji saini yake.


Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa sababu kubwa ya kuendelea kuwaongezea kandarasi nyota wao ni kuendeleza kikosi chenye nguvu ambacho kitakuwa na maelewano kwa muda mrefu.

Chirwa baada ya kusaini dili hilo amesema kuwa ataendelea kuwafurahisha mashabiki wa Azam FC kwa kufanya kazi yake kwa juhudi ndani ya uwanja.

Azam FC ikiwa imecheza mechi 28 kwenye msimamo ipo nafasi ya pili imefunga mabao 37 huku Chirwa akifunga mabao nane, pia kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho, Azam FC dhidi ya Lipuli bao la ushindi alifunga Chirwa

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.