BAKARI mwamnyeto, beki anayekipiga Coastal Union, dili lake la kutua Simba limeingiliwa kati na wapinzani wa jadi Yanga ambao wanahitaji huduma yake.
Beki huyo chipukizi alikuwa kwenye mpango wa muda mrefu na Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ambaye anahitaji kuboresha kikosi chake hasa kwenye safu ya ulinzi ambayo inaonekana kuwa na ubutu hasa linapokuja suala la kwenye michuano ya kimataifa.
Habari zinaeleza kuwa tayari mabosi wa Yanga chini ya GSM wameingia kati na kuanza harakati za kuwania saini ya beki huyo ambaye ni miongoni mwa wazawa wanaofanya vizuri.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mpango wa usajili kwa sasa hakuna ila kilichopo ni kufuatilia wachezaji wazuri ili wakati wa usajili ukifika mambo yasiwe magumu.
Mwamnyeto amesema kuwa amekuwa akiskia habari kwamba anahitajika ndani ya klabu za Simba na Yanga jambo analosubiria kuona likitokea.
"Nimekuwa nikiskia kwamba ninahitajika ndani ya Simba na Yanga, kwa kazi ambayo ninafanya ya kucheza mpira sina tatizo iwapo utaratibu utafuata," amesema.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, Coastal Union ikiwa imecheza mechi 28 safu yao ya ulinzi imeruhusu kufungwa mabao 19 ambapo ina wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 132
Post a Comment